Mmoja auawa katika ghasia za uchaguzi Kenya | Habari za Ulimwengu | DW | 07.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mmoja auawa katika ghasia za uchaguzi Kenya

NAIROB.Mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa huko magharibi mwa Kenya wakati makundi mawili yalipokutana kwenye harakati za kampeni za uchaguzi mkuu wa mwezi huu.

Polisi wamesema kuwa mtu huyo ambaye ni dereva wa tax aliuawa baada ya makundi mawili hasimu kukutana kwenye mikutano ya kampeni katika wilaya ya Kakamega kiasi cha kilometa 350 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Nairobi.

Kifo hicho kinafanya idadi ya waliyouawa toka mwezi Julai wakihusishwa na matukio ya uchaguzi kufikia watu 39.

Zaidi watu millioni 14 wamejiandikisha nchini Kenya kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani utakaofanyika tarehe 27 mwezi huu.

Kura za maoni za hivi karibuni zinaonesha kuwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga anaongoza kwa asilimia kidogo dhidi ya Rais Mwai Kibaki.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com