Mmlikaji wa mgodi wa mawe ahukumiwa miaka sita gerezani | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mmlikaji wa mgodi wa mawe ahukumiwa miaka sita gerezani

Shirika la habari la kitaifa la Xinhua nchini China limetangaza kwamba mahakama moja nchini humo imemuhukumu mwanamume mmoja anayemiliki mgodi wa makaa ya mawe ambao ulikumbwa na mlipuko na kusababisha vifo vya watu 171 miaka miwili iliyopita.

Mmilikaji wa mgodi huo amehukumiwa pamoja na maafisa wengine wanne wa kampuni yake.

Mahakama ya mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, imemhukumu mmlikaji huyo kifungo cha miaka sita gerezani huku maafisa wake wakiadhibiwa kifungo cha kati ya miaka mita unusu na miaka mitano.

Mlipuko uliotokea mwezi Novemba mwaka wa 2005 kwenye mgodi wa makaa ya mawe mjini Qitaihe ni mojawapo ya milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini China.

Migodi ya China inaelezwa kuwa hatari zaidi duniani huku takwimu rasmi zikionyesha kuwa wafanyakazi 4,700 katika migodi hiyo waliuwawa mwaka jana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com