Mkutano wa viongozi wa Afrika, wamalizika. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 04.02.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mkutano wa viongozi wa Afrika, wamalizika.

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika umemalizika leo mjini Addis Ababa, huku wajumbe wakiwa wamegawanyika kuhusu mpango wa mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, Muammar Gadhafi kuunda muungano wa Mataifa ya bara hilo.

Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni Kiongozi wa Libya, Kanali Moammar Kadhafi.

Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni Kiongozi wa Libya, Kanali Moammar Kadhafi.

Umoja wa Afrika ulimchagua kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi kuongoza umoja huo siku ya Jumatatu, licha ya wasiwasi mkubwa uliokuwepo miongoni mwa wanachama juu ya wito wake wa kuundwa kwa muungano wa mataifa ya Afrika.


Lakini viongozi na waakilishi kutoka nchi 53 wanachama , wakati walipokuwa wakikaribia kuhitimisha mkutano huo, mpasuko ulionekana kuongezeka hasa walipokuwa wakijadili ripoti, kuhusu njia za kuifanyia marekebisho jumuiya hiyo, hali ambayo pia ilisababisha kuongezwa kwa muda wa mkutano huo.


Bwana Gadhafi alitoka nje usiku wa manane jana bila ya kusema kitu chochote na baadaye viongozi wengine nao wakafuata asubuhi wakikubaliana tu kukutana tena baadaye.


Walipoulizwa baadhi ya viongozi wa Afrika, kuhusiana na hatua hiyo ya Mwenyekiti huyo mpya kuondoka wakati majadiliano bado yalikuwa yakiendelea, walitoa maoni tofauti, Huku rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf amesema kiongozi huyo hakutoka nje ila alikuwa amechoka.


Naye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Botswana Escala Mani, kwa mtazamo wake anasema hawezi kusema kwa nini alitoka nje, kwa vile alikuwa na Naibu wake ambaye aliendelea kumwakilisha, lakini anaweza kuwa alikuwa amechoka kwa vile alikuwa akiongoza kikao hicho kwa muda mrefu, hivyo alifikiria kutoka nje na kupumzika, lakini tuliweza kumaliza majadiliano kuhusu mapendekezo ya baraza la utendaji, mara tu alipoondoka, kitu ambacho kila mmoja alikubaliana nacho, yeyey ni mmoja wa wale ambao hawakukubali, , sio kwa sababu kulikuwa hakuna makubaliano ila walifikia makubaliano.


Mkutano huo pia ulikubaliana kupanua majukumu ya kamisheni ya Umoja wa Afrika na pia kubadili jina lake na kuwa Mamlaka ya Umoja wa Afrika, ingawa suala hilo la kubadili jina bado ni tete, miongoni mwa wanachama.


Kulingana na mwenyekiti huyo mpya Gaddafi, njia pekee ya kulisukuma mbele bara la Afrika linalozongwa na vita na ukame ni kuwa na shirikisho la bara zima.


Mtazamo wa mataifa mengine kama vile Nigeria,Afrika Kusini,Ethiopia na Kenya ni kutimiza fikra hiyo hilo hatua kwa hatua.
 • Tarehe 04.02.2009
 • Mwandishi Halima Nyanza/AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Gn9K
 • Tarehe 04.02.2009
 • Mwandishi Halima Nyanza/AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Gn9K
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com