Mkutano wa kilele kuhusu wakimbizi barani Ulaya | Magazetini | DW | 28.08.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mkutano wa kilele kuhusu wakimbizi barani Ulaya

Wahariri wa  magazeti  ya  Ujerumani leo(28.08.2017) wamejishughulisha na mkutano unaopangwa kujadili sera za wakimbizi barani Ulaya, kampeni za uchaguzi nchini  Ujerumani zapamba moto.

Gazeti  la Stuttgarter Nachrichten, kuhusiana  na mkutano  wa  kilele  wa  mataifa  manne  kujadili  sera  kuhusu wakimbizi barani  Ulaya limeandika.

"Katika  suala  hili  la  sera  za  wakimbizi, matarajio  ya  wananchi  ni makubwa  lakini  kwa  upande  wa  serikali  hali  ni  ngumu. Kwa  hiyo itavunja  moyo , kwa  atakayezungumzia  kupiga  hatua  zaidi  kuunga mkono  matamshi  ya  kansela  katika  mkutano  huo utakaohudhuriwa  na  viongozi  wa  Ufaransa, Italia na  Uhispania ambapo  watajumuika  na  kujadili  pamoja  na  viongozi  wa  mataifa jirani  ya  Ulaya  kutoka  Afrika  kaskazini. Kwa  kiasi  kikubwa  ndio yanahusika  na  taizo  hilo."

Gazeti  la  Badische Zeitung nalo  linazungumzia  kuhusu  mkutano huo , mhariri  anandika ...

Deutschland Merkel Statement zum Barcelona Anschlag (picture-alliance/dpa/M. Kappeler)

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

"Bila  shaka  kungekuwa  na  wahamiaji  haramu  wachache , iwapo bara  la  Afrika  halingekuwa  na umasikini, rushwa na  kutoheshimu haki , na  kusababisha  watu kuhatarisha  maisha  yao  kufanya safari  ya  hatari  badala  ya  kubaki  katika  mataifa  yao. Na  ni kutokana  na  hali  hiyo ya  kutokuwa  na  hakika  ya  maisha  yao ndio sababu wasafirishaji  haramu  wananufaika katika  kazi  yao hiyo. Kufikiria  njia  mbadala  ya kuwasaidia  watu  hawa  sio  jambo la  kijinga. Iwapo  kutakuwa  na  watu  wachache watakaofanyakazi hii  ya  kuwasaidia wahamiaji  kufanya safari  hizi , kutakuwa  pia wakimbizi  watakuwa wachache."

Kampeni za Uchaguzi Ujerumani

Kampeni  za  uchaguzi  nchini  Ujerumani  zinaingia  katika  hatua ya kuvutia  zaidi. Gazeti  la  Rheinpfalz , la  mji  wa  Ludwigshafen linazungumzia kuhusu  marufuku  ya  ushirikiano  katika  nyanja  ya elimu ..

"Kuondolewa  kwa marufuku  ya  ushirikiano, majimbo  ya  Ujeruimani yatapoteza  kitu  muhimu cha utambulisho  wao. Itakuwa  ujinga kufikiri , kwamba  serikali  kuu itoe malipo, na  serikali  za  majimbo zitimize zinayotakiwa  kutimiza. Hata  katika  maeneo  mengine serikali  za  majimbo  zimo  katika  mbinyo, uwezo  wake  umo hatarini."

Kuhusu  mada  hiyo  hiyo ya kampeni gazeti  la  Neue Osnabrücker Zeitung  linaandika  kuhusu  kashfa  ya  dizeli. Mhariri  anaandika kwamba  mwanzo mpambano  katika  kampeni  ulionekana  kutokuwa na  mvuto, lakini  sasa  hali inaanza kuwa  moto  moto, ikihusisha malumbano ya  kashfa  ya  dizeli.  Hakuna  mada  ambayo  ina  ncha nyingi  na  kuleta  hamasa  kwa  wananchi  kama  hii, na  katika ujumla wake  wanasiasa  wote  wamo. Wanapaswa  kulumbana kama  anavyofanya  Host Seehofer  wa  chama  cha  CSU  na  Cem Özdemir  wa  chama  cha  kijani. Tunasubiri  bado, hata hivyo mhariri anaandika, kuona  iwapo matamshi  ya  nani  yanaweza  kuzua malumbano  makubwa  zaidi.

Trump na wanazi mamboleo

Gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung , linaandika  kuhusu msamaha aliotoa  rais Donald Trump  kwa  sheriff Joe Arpaio, licha ya  kuhusishwa  na  kashfa  kadhaa za  kibaguzi. Mhariri  anaandika.

Donald Trump, Joe Arpaio (picture-alliance/AP PhotoM. Altaffer)

Rais Donald Trump na Joe Arpaio(kulia)

"Jela ya muda  iliyojengwa  kwa  mahema  ambayo  imetayarishwa na  kiongozi wa  eneo kwa  Marekani akijulikana  kama  Sheriff , Joe Arpaio  katika  jangwa  la  Arizona pamoja  na udhalilishaji aliotayarisha  dhidi  ya  jamii  ya  watu  wachache  nchini  humo, ni suala lililoshutumiwa kwa  kiasi  kikubwa  nchini  Marekani,  na  pia upinzani  alioonesha  seneta  kutoka  chama  cha  Republican John McCain  dhidi  ya  msamaha  uliotolewa  na  rais Trump kwa kiongozi  huyo. Kwa  hatua  ya  rais Trump  kumpa msahama kiongozi  huyo, amewapa  nguvu  wale  wenye siasa  kali  za mrengo  wa  kulia. Trump  amechukua  hatua  hiyo licha  ya  kesi inayomkabili  Arpaio mahakamani, na  hii inaonesha   jinsi  Trump asivyouheshimu  mfumo  wa  sheria  nchini humo."

Hayo  ndio baadhi  ya  maoni  ya  wahariri  wa  magazeti  ya Ujerumani  kwa  leo (28.08.2017). 

Mwandishi: Sekione  Kitojo  /  Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com