Mkutano wa Kikwete na waandishi habari
30 Oktoba 2010Matangazo
Mgombea wa kiti cha urais wa chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi-CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, jana usiku alikuwa na kipindi cha maswali na waandishi habari na kurushwa moja kwa moja na vyombo vya habari.
Kikwete alitetea kipindi chake cha miaka mitano madarakani, kwa kueleza kuwa hana wasiwasi wakati uchaguzi mkuu unafanyika hapo kesho, kwa sababu ana amini kwamba kiwango chake cha utendaji kinampa fursa nyingine ya miaka mitano.
Mpitiaji: Sekione Kitojo.