Mkutano kati ya Marekani na Iran | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.05.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mkutano kati ya Marekani na Iran

Mabalozi wa Marekani na Iran mjini Baghdad wamekutana leo kwa muda wa masaa 4.Haikutazamiwa kwamba wangetatua tofauti zao zote.Iran imedai Marekani itoe wakati wa kuondoa majeshi yao kutoka Iraq.

Kwenye mkutano kati ya mabalozi wa Marekani na Iran mjini Baghdad

Kwenye mkutano kati ya mabalozi wa Marekani na Iran mjini Baghdad

Mahasimu wakubwa-Marekani na Iran wamekuwa na mazungumzo ya uso kwa uso hii leo mjini Baghdad –ya kwanza katika daraja hii tangu kupita miaka 27.Katika kikao hichjo,Marekani imeitaka Iran kukomesha kuungamkoono wanamgambo wanaozusha machafuko nchini Iraq.

Iran nayo inadai vikosi vinavyoongozwa na Marekani nchini Iraq ndio chanzo cha balaa lote na inaituhumu Marekani, kuwaruhusu waasi wa Iran kuitumia Iraq kama kambi dhidi ya Iran.

Balozi mpya wa Marekani, mjini Baghdad, Ryun Crocker, ameeleza kwamba amekutana na balozi wa Iran mjini Baghdad, Hassan Kazemi kwa muda wa masaa 4 hii leo katika kikao cha kwanza kabisa katika daraja ya juu kama hii tangu nchi hizo mbili kuvunja mahusiano ya kibalozi 1980. Balozi wa Marekani, aliarifu kuwa alishikilia katika mazungumzo yao kwamba Iran ioneshe kivitendo kauli yake kuwa inaiungamkono serikali ya waziri mkuu al-Maliki kwa kuacha kuviungamkono vikundi vilivyoshika silaha nchini Iraq.

“Madhumuni ya mazungumzo yetu katika kikao hiki sio kujenga msingi wa mashtaka ya kisheria ,tukichukulia Iran inaelewa inayotenda, bali hoja yetu ni kusema tunajua pia kinachofanyika ni hatari kwa Iraq," alisema Crocker.

Balozi Crocker akasisitiza kwamba vitendo vya Iran lazima vilingane na kanuni zake inazohubiri.Akaongeza kusema kuwa katika kikao chao ,Iran imependekeza kuundwa Tume usalama ya pande 3 ikiwajumuisha wairaki wenyewe,wajumbe wa Marekani na Iran yenyewe-pendkezo ambalo balozi wa marekani amelikataa.

Crocker alisema wairani hawakushughulikia kabisa manunguniko ya Marekani isipokuwa wao wamelalamika kwa jumla kukaliwa Iraq na majeshi ya marekani na kudai kuwa Marekani haikufanya juhudi za kutosha kuvipa mafunzo vikosi vya Iraq.

Hakuwapo tangu mwanzo na matarajio kwamba wajumbe hao 2 wangeafikiana juu ya swali la balaa la Iraq.Kwani wizara ya nje ya Iran katika mkesha wa kikao hiki cha leo iliwatuhumu majasusi wa marekani kusimamia vitimbi vya uharibifu dhidi ya serikali ya Iran.

Marekani ikikanusha tuhuma kama hizo siku za nyuma lakini zabainisha wazi mwanya mkubwa wa tofauti katika uhusiano baina ya Teheran na Washington,kiasi cha robo-karne tangu pale wajumbe wa kibalozi wa marekani walipotekwsanyara ubalozini mwao kwa siku 444.

Mtangulizi wa balozi Crocker mjini Baghdad, Zalmay Khalizad ambae sasa ni balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alikwishabainisha nae wakati wa mkutano wa kimataifa juu ya Irak.mjini Baghdad, hapo Machi mwaka huu kuwa kikao cha leo haikingezaa matunda mema.Kwsani,aliituhumu wakati ule Iran kuviungamkono vikundi vya wanamgambo wanaopigana nchini Iraq.

Balozi huyo wa zamani wa Marekani alisema hivi wakati ule: "Kwanza, yatupasa kuangalia kinapita nini:je, silaha zaidi zavukishwa mpaka kuingia Iraq,kunatolewa msaada kwa wanamgambo au kwa vikundi vilivyoshika silaha?"

Hayo ndio mambo yanayotulazimu kuyaangalia ili kujua msimamo wa upande wapili….Kwani,hicho ndicho cha kuhesabika !”

Hatahivyo, balozi wa Marekani mjini Baghdad,Ryan Crocker, aliyaeleza mazungumzo yao kuwa ya maana wakati Iran imeitaka marekani kutoa muda wa kuondoa majeshi yake kutoka Iraq.

Huku wajumbe hao wa kibalozi wakizungumza, bomu liliripuka mjini Baghdad na kuua watu 19 na kuwajeruhi wengine kiasi cha 40 hii leo.

Hii ilitokea baada ya wanamgambo kuyatekanyara mabasi 2 katika shina la Baghdad na kuwanyakua kiasi cha abiria 15 kwa muujibu wa polisi ilivyoarifu.Si chini ya polisi 3 ni miongoni mwa waliouwawa.

Mapigano yalianza baada ya polisi kuwasili mahala hapo yalipotekwa nyara mabasi hayo nusu saa baadae.Wapiganaji 9 walikamatwa wakati wakivihujumu vikosi vya usalama.Kiasi cha ndege 2 za helikopta za kimarekani zikiruka juu ya eneo hilo,lakini hazikushiriki moja kwa moja mapiganoni.

 • Tarehe 28.05.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB3v
 • Tarehe 28.05.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB3v
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com