Mkondo wa Obama Mashariki ya Kati utaishia wapi? | Magazetini | DW | 28.01.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Mkondo wa Obama Mashariki ya Kati utaishia wapi?

Ikibidi atatumia nguvu dhidi ya Iran ?

Obama na makamo Biden

Obama na makamo Biden

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo yametuwama zaidi juu ya kumbukumbu ya msiba wa kuhilikishwa wayahudi katika vita vya pili vya dunia-Holocaust,mkondo unaofuatwa na Rais Barack Obama wa Marekani kufumbua kitandawili cha mgogoro wa Mashariki ya Kati na mpango wapili wa serikali ya Ujerumani wa kuustawisha uchumi .

Ilikua tena zamu ya Ramadhan ali kuwakagulia safu hizo za wahariri na anaanza na gazeti la ABEND ZEITUNG juu ya msiba wa kuhilikishwa wayahudi.Laandika:

"Mtu aweza kuelewa kwanini Bibi Charlotte Knobloch na Baraza kuu lake la wayahudi , wamesusia kikao maalumu cha kukumbuka maafa hayo katika Bunge la Ujerumani -Bundestag......Laskini,sehemu kubwa ya wayahudi na wasio wayahudi, wanaishi humu nchini wakijua yaliopita katika historia na juu ya hivyo, wanaishi pamoja bila udhia.Na hii ni muhimu zaidi kuliko malalamiko yoyote katika jukwaa la siasa."

Gazeti la FINANCIAL TIMES la Ujerumani, linauangalia mkondo anaofuata Rais Barack Obama juu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati.Linaandika:

"Kwa kadiri gani mkondo wa kusikiliza kila upande utaleta maendeleo katika mzozo wa Mashariki ya kati na juu ya Iran ,kwa sasa haijulikani. Upole anaonesha sasa Obama haubainishi, vipi atafanya pale itakapombidi kupitisha uamuzi mgumu . Obama anasisitiza mshikamano wa Marekani na Israel.Kuhusu Iran, anaazimia kutumia ala zote ilizonazo Marekani pamoja na diplomasia.Silaha nyengine mfano wa nguvu za kijeshi,haondoi uwezekano wa kuitumia."

Ama gazeti la Rhein-Necker-Zeitung kutoka Heidelberg linauchambua mpango wapili wa serikali ya Ujerumani wa kustawisha uchumi.Laandika:

"Bila shaka, Kanzela na mshirika wake waziri wa fedha Steinbruck,

wanaupigia debe mpango wao wa kuustawisha uchumi uliodorora.Lakini, katika anga la uchumi wa dunia ,wanarandia mwewe (wala mizoga.)....Kwa mara ya kwanza takriban nchi zote za kiviwanda, zinatumbukia kwenye mtego wa kuja kunaswa na madeni.

Msiba huu kwanza utazisukuma ukingoni mwa janga la kufilisika nchi za Umoja wa Ulaya kwavile, hakuna tena aliyetayari kubeba madeni yao.

Kwenye kona, ughali wa maisha unachungulia hata katika nchi zinazotumia sarafu ya Euro.Jambo moja tu ni la uhakika:Mwishoe,raia ndie atakaelipa gharama. "