1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Migogoro yachochea mauzo makubwa ya silaha ulimwenguni

1 Desemba 2025

Mashirika yanayotengeneza silaha ulimwenguni yalifikia viwango vya juu vya mapato mwaka 2024, vilivyochochewa na vita na mizozo ya kisiasa.

https://p.dw.com/p/54Xpp
Urusi | Mfumo wa kombora wa Iskander
Mauzo ya silaha yameongezeka kutokana na mahitaji makubwa yanayochochewa na migogoro ulimwenguniPicha: Russian Defense Ministry Press Service/AP Photo/picture alliance

Kulingana na takwimu zilizotolewa Jumatatu na Taasisi ya Utafiti wa Amani ya Kimataifa ya Stockholm (SIPRI), kampuni 100 kubwa zaidi ulimwenguni ziliongeza mapato yao ya pamoja kutokana na mauzo ya silaha na huduma nyingine za kijeshi kwa asilimia 5.9 mwaka uliopita na kufikia takriban dola bilioni 679, hiyo ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kuwahi rekodiwa.

SIPRI imesema mahitaji ya silaha yamechochewa kimsingi na vita nchini Ukraine na Gaza, mizozo inayoongezeka ya kikanda ya ulimwenguni, na vilevile ongezeko la matumizi makubwa ya fedha katika shughuli za kijeshi

Marekani ndiyo inaongoza ikiwa na kampuni 39 kati ya kampuni 100 za mauzo ya silaha.