Michezo ya Olympic-rekodi za dunia zavunjwa | Michezo | DW | 11.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo ya Olympic-rekodi za dunia zavunjwa

Siku ya tatu ya mashindano ya Olympic imeshuhudia rekodi nne za dunia zikivunjwa huku,muogeleaji wa Marekani Michael Phelps akijiwinda kuchukua medali nane za dhahabu katika mashindano hayo.

default

Nicole Cooke wa Uingereza akionesha medali yake ya dhahabu aliyoshinda katika mbio za baiskel kwenye michezo ya Olympic mjini Beijing hapo jana

Phelps huku akishuhudiwa na Rais George Bush aliyeoondoka leo huko China kurejea nyumbani alifanikiwa kushinda medali ya pili ya dhahabu katika nchezo huo na sasa amebakisha medali sita kuvunja rekodi ya mmarekani mwenziye Mark Spitz aliyoiweka katika michezo ya Olympic mjini Munich hapa Ujerumani mwaka 1972 ambapo alitwaa medali saba za dhahabu katika mchezo huo wa kuogelea.


Ama kwa upande wa Afrika Zimbabwe ilikuwa nchi ya kwanza kutwaa medali baada ya muogeleaje wake  Kirsty Coventry kutwaa medali ya fedha.


Nchi nyingine ni Algeria ambayo imepata medali ya shaba.


Katika masumbwi bondia kutoka Kenya Nicolaus Okoth  anapanda ulingoni muda mfupi ujayo kupambana na Reyes Aturo kutoka Mexico katika uzito wa feather.


China  ndiyo inayoongoza mpaka sasa ikiwa na medali kumi 11 dhahabu nane, tatu fedha, ikifuatiwa na Marekani yenye medali 12 tatu dhahabu, nne fedha na tano shaba.


Ujerumani mpaka sasa imekusanya medali mbili moja fedha na moja shaba.


Katika mchezo wa kulenga shabaha Abhinav Bindra aliipatia India medali ya kwanza ya dhahabu ikiwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji binafsi kufanya hivyo toka mwaka 1928.Ingawaje timu ya hockey ya nchi hiyo imewahi kushinda medali ya dhahabu mara nane mara ya mwisho ikiwa mwaka 1980.


Ushinda wa Bindra ulisimamisha kila kitu nchini india ambapo katika mji wa Chandigarh anakotoka mama yake alisema kuwa sasa mwanaye amekuwa mvulana mwenye hadhi miongoni mwa mabinti wa India.


Katika kandanda hapo jana timu za Afrika zilitamba ambapo Nigeria iliitandika  Japan mabao 2-1, hukuCameroon ikiifunga Honduras bao 1-0, nayo Ivory Coast ikipata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Serbia.


Nahodha wa Brazil Ronaldinho aliiongoza timu hiyo katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya New Zeland na kufuzu kwa robofainali.


Wenyeji China waliwekwa katika ncha ya kuyaanga mashindano hayo baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Ubelgiji hivyo sasa inawajibika kuifunga Brazl ili kukata tiketi ya robofainali.


Ama nje ya viwanja vya michezo hiyo, mwendesha baiskeli wa kike kutoka Uhispania amekuwa mwanamichezo wa kwanza kubainika kutumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu


Mwendesha baiskeli huyo Maria Isabel Moreno ametimuliwa kutoka katika mashindano hayo na tayari amekwishareja nyumbani.Rais wa chama cha mchezo  huo duniani Pat McQuad alisema kuwa hiyo ni pigo kwa mchezo huo.

 • Tarehe 11.08.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Eui0
 • Tarehe 11.08.2008
 • Mwandishi Liongo, Aboubakary Jumaa
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Eui0
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com