1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombea Urais nchini Urusi, Medvedev azungumza na viongozi wa bunge

Halima Nyanza11 Desemba 2007

Mgombea wa Urais kupitia chama tawala nchini Urusi, Dmitry Medvedev, amekutana kwa mara ya kwanza na viongozi wa bunge la nchi hiyo, tangu alipotajwa kuwa mrithi wa Rais Putin, katika uchaguzi utakaofanyika mwakani.

https://p.dw.com/p/Ca6o
Mgombea Urais nchini Urusi, kupitia chama tawala, Dmitry Medvedev.Picha: AP

Akizungumza mjini Moscow, mgombea huyo wa ,kiti cha Urais nchini Urusi kupitia chama tawala, ambaye pia ni Naibu wa kwanza wa Waziri Mkuu, Dmitry Medvedev, amesema moja ya mambo atakayotilia umuhimu pindi atakapokuwa madarakani ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi hiyo kwa manufaa ya raia wa nchi hiyo.

Ameeleza kuwa wanahitaji kubadili mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana nchini humo katika kipindi cha miaka minane iliyopita kuweza kunufaisha jamii ya nchi hiyo kitendo, ambapo anakiri kuwa mwezie anayeondoka madarakani tayari alishaanza.

Aidha ameahidi kuimarisha uhusiano kati ya uma na serikali, ambapo amekiri kuwa uhusiano si mkubwa kati ya uma na mamlaka, na kwamba suala hilo ni tatizo hivyo watajaribu kurekebisha hali hiyo.

Kauli hiyo ni taarifa ya kwanza kwa Medvedev kuitoa kwa umma tangu Rais Vladmiri Putin alipomtaja siku ya Jumatatu kuwa ndiye mrithi wake.

Medvedev ambaye ni mtu wa karibu wa Rais Putin anaelezwa pia ni miongoni mwa watu waliomsaidia Putin kwenye kampeni za Urais mwaka 2000.

Baadhi ya wanasiasa na wachunguzi wa mambo nchini humo wamemuelezea Medvedev kuwa ni mtu makini na mwenye uzoefu na mambo mengu kama anavyoeleza mwanaharakati Sergey Mironov kutoka Urusi.

‘’Medvedev ni mwanasheria mzuri ambaye anafahamu sheria za umma na za kimataifa pamoja na kuwa na ujuzi katika masuala ya kimataifa, amefanya kazi katika ofisi ya Rais pia muda mrefu amefanya kazi katika wizara ya ulinzi hvyo anaufahamu mkubwa katika maeneo ya ulinzi na mambo ya ndani.

Naye Michail Barsschevsky kutoka chama cha Nguvu ya Wananchi alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na Mgombea huyo wa Urais aliyetangazwa na Rais Putin nchini Urusi,

’’Ni kjana ana mwenye mwelekeo wa kidemokrasia na nina uhakika kwamba chini ya uongozi wake tutaendelea zaidi pia tukizingatia kujenga taifa la haki na kidemokrasia’’.

Rais Vladmir Putin anamaliza muda wake wa uongozi nchini humo mwezi Machi mwakani, mwezi uliopita alitoa hotuba nzito kwa wananchi wakati wa kampeni za ubunge kueleza mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika vipindi vya uongozi wake.