1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Medvedev atawazwa kama rais mpya wa Urusi

Kalyango Siraj7 Mei 2008

Waziri mkuu ajiuzulu

https://p.dw.com/p/Dv0k
Dmitry Medvedev rais mpya wa Urusi ameapishwa rasmi jumatano katika sherehe iliofanyika Kremlin Moscow.Picha: AP

Rais wa tatu wa Urusi tangu kusambaratika kwa Umoja wa Soviet,Dmitry Medvedev ameapishwa.Medvedev amechukua nafasi ya Vladimir Putin ambae muhula wake ulimalizika.Sherehe imefanyika leo katika jumba la Kremlin mjini Moscow.

Dimitry Medvedev mwenye umri wa miaka 42 amekula kiapo cha kuwa rais wa Urusi jumatano mjini Moscow mji mkuu wa taifa hilo. Amekula kiapo cha kuwa kiongozi wa tatu wa nchi hiyo tangu Umoja wa Soviet usambaratike mwaka wa 1991,katika ukumbi wa Andreyevsky.

Sherehe hiyo iliofanyika Kremlin imehudhuriwa na wageni waalikwa zaidi ya elf mbili,na pia mamilioni ya watu ulimwenguni waliokuwa wanaifuatilia kupitia televisheni.

Katika hotuba yake ya kwanza kama rais wa rais Medvedev amesema kuwa atayapa kipaumbele masuala ya kulinda uhuru wa wananchi pamoja na uchumi.

Kabla ya hapo,mtangulizi wake Vladimir Putin,alitoa hotuba fupi ambapo aliwashukuru raia wa Urusi kwa msaada wao na pia kukubali awamu zake mbili ofisini.

Medvedev mwenye umri wa miaka 42,ataanza rasmi kazi zake rasmi kama rais hapo kesho alhamisi wakati atakapo mteua mtangulizi wake Putin, mwenye miaka 55, kama waziri mkuu.Kwa mantiki hiyo aliekuwa waziri mkuu Viktor Zubkov amejiuzulu.

Hatua hiyo huenda ikazusha dukuduku la kutaka kujua nani mwenye uamuzi mkubwa katia dola lenye uwezo mkubwa wa kijeshi pamoja na uchumi wa thamani ya dola za kimarekani zaidi ya mabilioni kadhaa.

Warusi zaidi ya theluthi mbili,kwa mujibu wa uchguzi uliofanywa na kituo kinachojitegemea cha Independent Levada Centre, wanaamini kuwa Putin ataendelea na udhibiti wake wa dola.

Sherehe za jumatano zimemfanya Putin kuwa kiongozi rasmi wa chama tawala cha United Party,hali itakayomfanya kuongoza chama chenye usemi mkubwa bungeni ambacho kinaweza hata na kupitisha mageuzi ya katiba ya nchi.

Putin alilazimika kujiuzulu kutokana na masharti ya katiba ya nchi na hilo kumfanya kiongozi wa kwanza wa Urusi kucha madaraka kwa hiari.

Sherehe za leo pia zimeifanya Urusi kuwa taifa ambalo linaonekana kuongozwa na watu wawili.

Medvedev ni wakili na ni shabiki wa kundi la muziki la Uingereza la Deep Purple.