1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa fedha wa G7 wakutana Italia

24 Mei 2024

Mawaziri wa fedha wa nchi zilizositawi kiviwanda (G7) wameanza mkutano wa siku mbili nchini Italia kujadili haja ya kuipa Ukraine mkopo na kupinga sera za kiviwanda za China wanazodai "zimekosa usawa."

https://p.dw.com/p/4gFtG
Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen.
Waziri wa Fedha wa Marekani, Janet Yellen.Picha: Kazuhiro Nogi/Pool/AP/picture alliance

Kuelekea mkutano huo ulioanza Ijumaa (Mei 24) mjini Stresa kaskazini mwa Italia, waandaaji walionesha hakutakuwa na ugumu kwenye shinikizo hilo la Marekani kuipa Ukraine mkopo kwa kuzingatia mapato ya baadaye kutokana na baadhi ya mali za Urusi za thamani ya dola bilioni 300 ambazo umoja huo umezizuia.

Soma zaidi: Waziri wa fedha wa Marekani ahimiza mipango kabambe kwa mali za Urusi

Akizungumza na waandishi habari kabla ya kikao cha ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire alisema wangelipendekeza kutumia faida itakayotokana na mali za Urusi kwa miaka ijayo,

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen, amesema mkopo huo unaweza kuwa kima cha dola bilioni 50, lakini bado hakuna kiwango rasmi ambacho kimeafikiwa.

Soma zaidi: G7 inahitaji kusimama pamoja kudhibiti ukuaji wa China kiviwanda

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Christian Lindner aliwaambia waandishi wa habari leo kwamba kundi la G7 sasa linajadili pendekezo la mkopo "kisheria" ingawa "masuala mengi ya kisheria na kiufundi bado hayajatatuliwa."