1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 inahitaji kusimama kudhibiti ukuaji wa China kiviwanda

22 Mei 2024

Waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire, amesema kundi la nchi tajiri kiviwanda G7, linapaswa kuungana pamoja kukabiliana na ushindani mkubwa wa China katika sekta ya viwanda muhimu ikiwemo sekta ya magari ya umeme.

https://p.dw.com/p/4g9Xg
Uswisi Stockholm |  Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Ulaya |  Bruno Le Maire, Ufaransa
Waziri wa Fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire, akizungumza wakati wa mkutano usio rasmi wa Umoja wa Ulaya kati ya mawaziri wa fedha wa umoja huo, Aprili 28, 2023.Picha: TT News Agency/Caisa Rasmussenvia REUTERS

Le Maire ameyasema hayo kabla ya kuanza mkutano wa kundi hilo nchini Italia siku ya Ijumaa na Jumamosi wiki hii.

Waziri huyo wa fedha wa Ufaransa amesema kundi la G7 pia linapaswa kuwa na msimamo wa pamoja juu ya mali za Urusi zinazozuiwa na kwamba Ufaransa iko tayari kufanyia kazi pendekezo la Marekani kutumia mali hizo kuipa mkopo Ukraine.

Wakati tofauti ya kiuchumi kati ya Ulaya na Marekani ikizidi kukuwa, Le Maire amesema pia Ulaya inahitaji kuondokana na hali ya kujikokota kiuchumi na kukuza mara dufu viwango vyake vya  ukuaji katika miaka kadhaa ijayo.