Matumaini ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uganda | Habari za Ulimwengu | DW | 30.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Matumaini ya kumalizika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uganda

Kampala:

Serikali ya Uganda na waasi wa LRA wameidhinisha awamu ya tatu ya makubaliano ya amani ya awamu tano,kwa lengo la kumaliza miaka 20 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.Duru za kuaminika toka pande hizo mbili zimesema hii leo.Pande hizo mbili zimetiliana saini makubaliano yanayotanguliza mbele “wajib na suluhu” kama malengo ya mazungumzo ya amani ya Juba”kusini mwa Sudan.Kwa mujibu wa wapatnishi ,makubaliano hayo yanalenga kuingiza mifumo ya jadi ya kuifumbua mizozo katika mfumo wa sheria wa Uganda.”Jana usiku tumetia saini kifungu nambari tatu kuhusu wajib na suluhu na hivi sasa tutaanza majadiliano ya namna ya kutia njiani makubaliano hayo “amesema hayo msemaji wa LRA Godfrey Ayoo.Msemaji wa ujumbe wa serikali ya uganda kepteni Barigye Ba-Hoku amesema kwa upande wake tunanukuu”makubaliano yamefikiwa baada ya majadiliano makali.”Mwisho wa kumnukuu kepteni Ba-Hoku aliyeyataja makubaliano hayo kua ni “hatua muhimu”.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com