1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema hakuamuru uvamizi dhidi ya waasi wa kikurdi

17 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CciM

Marekani imekanusha madai kwamba iliidhinisha mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Uturuki dhidi ya waasi wa kikurdi kaskazini mwa Irak. Hata hiyo maafisa wa Marekani wanasema walijulishwa kabla mashambulizi hayo kufanywa.

Matamashi hayo ya Marekani yametolewa baada ya jenerali wa jeshi la Uturuki kunukuliwa akisema serikali ya mjini Washington iliifungua anga ya Irak kwa Waturuki, ishara kwamba Marekani iliidhinisha harakati hiyo ya kijeshi. Mashambulizi hayo ya mpakani yalilenga ngome za waasi wa PKK, ambapo mtu mmoja aliuwawa.