1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuichangia Ukraine kijeshi dola milioni 300

13 Machi 2024

Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon itatoa msaada silaha wenye thamani ya dola milioni 300 kwa Ukraine, licha ya kuwa jeshi lenyewe kwa upande wake bado linakabiliwa na ukata wa fedha.

https://p.dw.com/p/4dS8h
Marekani Washington | Naibu Waziri wa Ulinzi Kathleen Hicks
Naibu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Kathleen Hicks akizungumza wakati wa mkutano na wanahabari Pentagon, Alhamisi, Novemba 2, 2023, Washington.Picha: Alex Brandon/AP/picture alliance

Na linahitaji angalau dola bilioni 10, ili kufidia silaha zote ambazo imezitoa kwenye akiba yake na kuisaidia Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.

Huo utakua ni msaada wa kwanza wa kiusalama kutangazwa na Pentagon kwa Ukraine, tangu Desemba ambapo maafisa walitamka hadharani kuwa hawana uwezo kwa kuisaidia zaidi kutokana na kutokua na akiba inayojitosheleza.

Taarifa ya jeshii kwa vyombo vya habari zinasema, msaada huo ni kama wa mara moja, ikaongeza kusema kuwa ni mpaka pale bunge litakapopitisha muswada wa matumizi ya ziada, ambao utajumuisha hadi dola bilioni 60 za misaada ya kijeshi kwa Ukraine kwa ajili ya makombora ya kudungua ndege, mizinga na silaha.

Tangazo la msaada huo linatolewa wakati kiongozi wa Poland, President Andrzej Duda yuko mjini  Washington kwa ajili ya kuishinikiza Marekani kuondosha vizingiti katika kuichangia Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi.