1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Jeshi la Ukraine ladungua droni 35 kazi ya 39 za Urusi

Lilian Mtono
10 Machi 2024

Jeshi la Ukraine limesema Jumapilii hii kwamba mifumo yake ya kujilinda angani imezuia mashambulizi 35 kati ya 39 ya droni zilizorushwa na Urusi kwa usiku mzima.

https://p.dw.com/p/4dM9n
Ingawa mashambulizi ya droni yanashika kasi kwa sasa, lakini bado mashambulizi ya ardhini yanaendelea
Mwanajeshi wa Ukraine akilfanya mashambulizi kuelekea eneo la Urusi wakati vita kati ya mataifa hayo jirani vikiendelea huko Oblast, Donesk. Picha hii ilipigwa Februari 14, 2024.Picha: Jose Colon/Anadolu/picture alliance

Jeshi hilo la Ukrain limesema kupitia ukurasa wa Telegram kwamba droni nyingi ziliharibiwa katika eneo la mashariki mwa Ukraine na kwenye mikoa ya kusini, ingawa haikuelezea kama kulitokea athari zozote.

Aidha limesema, Urusi ilifyatua makombora ya S-300 ingawa halikuweka wazi kama makombora hayo yalifika kwenye maeneo yaliyolengwa.

Taarifa nyingine kutoka mjini Kyiv hii leo zimesema shambulizi la Urusi katika mji wa Myrnograd, ulioko Donesk mashariki mwa taifa hilo limejeruhi karibu watu 9.