Mahakama Kuu yaunga mkono hali ya hatari | Habari za Ulimwengu | DW | 23.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mahakama Kuu yaunga mkono hali ya hatari

Mahakama Kuu nchini Pakistan imeunga mkono utawala wa hali ya hatari uliotangazwa na Rais Jemadari Pervez Musharraf tarehe 3 Novemba.Uamuzi wa mahakama hiyo umepitishwa siku moja baada ya Jumuiya ya Madola kwa mara ya pili kusitisha uanachama wa Pakistan katika kundi hilo la makoloni ya zamani ya Uingereza.

Siku ya Alkhamisi,mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola walichukua hatua hiyo wakisema, Pakistan imekiuka maadili ya kimsingi ya jumuiya hiyo.Kwa upande mwingine,waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif,anaeishi uhamishoni nchini Saudi Arabia,amesema kuwa hivi karibuni atarejea Pakistan kugombea uchaguzi wa bunge unaotazamiwa kufanywa mapema mwezi Januari.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com