LOS ANGELES : Kundi la Senegal lapata tuzo ya Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 15.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LOS ANGELES : Kundi la Senegal lapata tuzo ya Marekani

Kundi linalojishughulisha na elimu la Senegal lenye kupiga vita mila ya ukeketaji wa wanawake barani Afrika limejishindia tuzo ya Marekani ya Wakfu wa Kibinaadamu wa Conrad Hilton yenye thamani ya dola milioni moja na nusu.

Taasisi hiyo ya kujitegemea imewatunuku tuzo hiyo kwa kundi la Tostan ambalo hujishughulisha na kuelimisha watu juu ya madhara ya mila hiyo pamoja na masuala mengine ya kijamii na afya.

Wakfu huo wa Conrad Hilton umesema katika taarifa kwamba kwa kupitia vipindi vya elimu katika lugha za kienyeji Tostan imetowa ufumbuzi mkubwa,imewawezesha wanawake na kuboresha maisha kwa mamilioni ya watu katika nchi tisa za Afrika ambapo vijiji vimeweza kupunguza vifo vya watoto wachanga na vifo vya uzazi,kukomesha ukatili wa majumbani,kuboresha huduma za afya na lishe na kuboresha elimu kwa watoto wao.

Takriban wasichana milioni mbili hukabiliwa na ukeketaji kila mwaka hususan barani Afrika.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com