1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mo Ibrahim

Wakfu wa Mo Ibrahim ni taasisi ya Kiafrika ilioasisiwa 2006, lengo lake kuu likiwa: Kuangazia umuhimu wa utawala na uongozi barani Afrika kwa imani kuwa utawala na uongozi ndiyo msingi wa maisha bora kwa raia wa Afrika.

Taasisi ya Mo Ibrahim imekuwa ikijihusisha na utoaji wa tuzo ya kiongozi bora kwa marais wastaafu wa Kiafrika wanaokidhi vigezo vilivyowekwa, hutoa faharasi ya utawala bora barani Afrika ikiwa ni pamoja na utendaji wa mataifa kiuchumi na kijamii. Pia huandaa jukwaa la kila mwaka la Mo Ibrahim ambapo washiriki hujikita katika suala moja lwenye umuhimu wa kipekee kwa Afrika ambalo hufanyika katika nchi tofauti kila mwaka. Ukurasa huu ni mkusanyiko wa maudhui za karibuni za DW kuhusu Wakfu wa Mo Ibrahim.

Onesha makala zaidi