LONDON:majeshi ya mfungamano yanakaribia kuukimbia mji wa Basra? | Habari za Ulimwengu | DW | 19.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:majeshi ya mfungamano yanakaribia kuukimbia mji wa Basra?

Mshauri wa kijeshi wa Marekani amesema huenda majeshi ya Uingereza yakaondoka mji wa Basra,kusini mwa Irak katika namna ya kuumbuka.

Mshauri huyo bwana Stephen Biddle ambae ni mjumbe wa baraza la Marekani linaloshughulikia uhusiano wa nchi za nje ameliambia gazeti la Sunday Times la Uingereza kwamba majeshi ya mfungamano hayana tena uwezo wa kuudhibiti mji huo.

Ameeleza kuwa wapinzani ndiyo wenye usemi katika mji wa Basra na pana uwezekano wa majeshi ya mfungamano kutimuliwa kutoka kwenye mji huo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com