1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Nawaz Sharif atagombea uchaguzi Pakistan

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUF

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan,Nawaz Sharif anaeishi uhamishoni nchini Uingereza amesema, atarejea Pakistan tarehe 10 mwezi wa Septemba. Alipozungumza mjini London alisema,atatoa changamoto kwa kiongozi wa kijeshi wa Pakistan, Rais Pervez Musharraf,katika uchaguzi ujao.

Nawaz Sharif amesema,pamoja na umma wa Pakistan watapigana vita vyao kila mahala-barabarani na mahakamani-kwa sababu wanaamini kuwa huu ni wakati ulio muhimu kwa Pakistan na nchi hiyo lazima iondoshe udikteta kwa milele.

Majuma manne yaliyopita,Mahakama Kuu ya Pakistan iliamua kumruhusu Nawaz Sharif kurejea nyumbani. Sharif alipinduliwa na jeshi mwaka 1999.