KOMBE LA ULYA 2012 KUANDALIWA NA TALI ? | Michezo | DW | 17.04.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

KOMBE LA ULYA 2012 KUANDALIWA NA TALI ?

Kura inapigwa leo huko Cardiff,Wales kuamia ama Itali,Ukraine,Poland au Hungary na Croatia zitaandaa kombe la Ulaya 2012. Wataliana wanatarajiwa kutoroka na tiketi hiyo.

Fujo la mashabiki wahuni huenda likainyima leo Itali,mabingwa wa dunia nafasi ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Ulaya la mataifa 2012.hatahivyo, wengi wanatazamia uamuzi leo utaangukia mikononi mwa mabingwa hao wa dunia utakapokatwa huko Cardiff,Wales.

Kura imepigwa mapambano ya finali za makundi A/B/C kanda ya Afrika kuania tiketi za dimba la olimpik.

Kura imepigwa jinsi timu za Afrika zitakavyoumana kaunia nafasi za mwisho za dimba la olimpik 2008 kwa kanda ya Afrika:

Kantika kundi A:kuna Ethiopia,Ghana,Nigeria na Afrika Kusini.

Kundi B:Tembo wa Ivory Coast,Mali,Senegalna Zambia.

Kundi C linazikutanisha Botswana,simba wa nyika-Kameroun,Guinea na Morocco.Changamoto hizi za kuania tiketi za Olimpik zitachezwa chini ya mfumo wa Ligi kati ya March na Juni mwakani na washindi 3 kutoka kila kundi wataiwakilisha Afrika katika dimba la Olimpik mjini Beijing,hapo mwakani.

Kocha wa Arsenal London, Arsene Wenger ameelezea matumaini kwamba kipa wa taifa wa Ujerumani Jens Lehmann atarefusha mkataba wake na Arsenal. Mkataba wa Lehmann, mwenye umri wa miaka 37, unamalizika mwishoni mwa msimu huu.Lehmann akivumishwa kurudi katika Bundesliga-Ligi ya Ujerumani na kujiunga na Hertha Berlin.Wenger kocha wa Arsenal anatumai lakini kumbakisha Arsenal.

Stadi wa Werder Bremen inayosimama nafasi ya pili katika ngazi ya Ligi ya Ujerumani,Torsten Frings amekutana na waakilishi wa Juventus ya Itali kuzungumzia uwezekano wa kujiunga na viongozi hao wa serie B.Frings alikuwa Turin hapo jumatatu.

Nae Peter Crouch,mshambulizi wa FC Liverpool itayocheza nusu-fianli ya champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya,amekanusha fununu kuwa eti anataka kuiacha mkono Liverpool.

Liverpool inateremka leo uwanjani kucheza na Middlesborough pamoja na Crouch.Hatahivyo,jina lake limekuwa likifungamanishwa sana na klabu ya Newcastle.

Leo itapigwa kura huko Cardiff,Wales, kuamua ni taifa gani litaandaa Kombe la Ulaya la Mataifa 2012.

Mabingwa wa dunia Itali wanapigiwa upatu kutoroka na tiketi hiyo na wamejiandaa kujitembeza hii leo.

Wataliana lakini wana dosari moja ambalo laweza likawanyima tiketi hiyo-fujo la mashabiki wake wahuni.

Itali inawasili Cardiff leo na ujumbe wa watu 31 ukiongozwa na Giancarlo Abete,rais mpya wa shirikisho la dimba la Itali.Mataifa mengine yanayonyan’ganyia nafasi hiyo leo ni Poland,Ukraine na ombi la pamoja la hungary na Croatia.

Itali iliandaa kombe la Ulaya 1968 waliposhinda na wakaandaa tena 1980.

Bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia yam bio za marathon wanawake-Tegla Laroupe anakabiliwa nyumbani Kenya na deni la kodi ya mapato la Kenya Sh.milioni 11 sawa na dala 160,600-hii ni kwa muujibu wa afisa wa idara ya kodi.

Deni hilo latokana na nyumba zake anazokodisha kwa mwaka 1994 na 2000.

Tecla Laroupe mwenye umri wa miaka 33 sasa,alistaafu 2001 na sasa ni balozi wa UM katika michezo.

 • Tarehe 17.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHcL
 • Tarehe 17.04.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHcL