Mazoea ya wengi ni kwamba lugha zinazotumika kama kiunganisho cha watu wenye lugha tafauti za asili (linguafranca) ni lugha za Ulaya kama Kiingereza, Kihispania na Kifaransa kwa Waafrika, lakini sio lugha za Kiafrika.
Mohammed Khelef anazungumza na watu ambao si Waafrika wala Waswahili kwa asili zao, lakini wanatumia Kiswahili kama lugha ya kuwasiliana wao kwa wao, huku kila mmoja akitokea lugha tafauti na mwenzake: Kelly Askew kutoka Marekani, Mikhail Goromov kutoka Urusi na Uta Reuster-Jahn kutoka Ujerumani.
Kusikiliza makala hii, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.