KISMAYO:Raia wa Uholanzi arejeshwa Somalia na kuachiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 17.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KISMAYO:Raia wa Uholanzi arejeshwa Somalia na kuachiwa

Raia mmoja wa Uholanzi mwenye asili ya Kisomali aliyerejeshwa nchini Somalia baada ya kukamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi wa Kenya ameachgiwa huru.Mtu huyo alisisitiza kuwa hana uhusiano wowote na wapiganaji wa kiislamu katika taifa hilo la eneo la pembe ya Afrika linalozongwa na vita.Abdirizak Farah Ali raia wa Uholanzi aliye na asili ya Kisomali alierejeshwa Somalia hapo jana baada ya kuzuiliwa kwa siku kadhaa nchini Kenya.Kulingana na mtu huyo jamaa wa ukoo wake walihakikisha kuwa hakukamatwa tena na maafisa wa usalama baaada ya kuwasili mjini Mogadishu.

Maafisa wa serikali ya Somalia hawajatoa kauli yoyote kuhusu suala hilo nab ado haijabainika iwapo uongozi ulinuia kumkamata baada ya kuwasili mjini humo.Abdirizak Ali hakushtakiwa kwa kosa lolote alipozuiliwa nchini Kenya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com