KINSHASA:Wanajeshi Tisa wauwa na wafuasi wa Nkunda
30 Agosti 2007Matangazo
Wanajeshi tisa wa Kongo wameuwawa baada wanamgambo wanaomuunga mkono Kiongozi wa waasi Laurent Nkunda kuwashambulia huko mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini.
Takriban wanamgambo 900 waliwavamia wanajeshi wa serikali katika eneo la Rubaya kiasi kilomita 60 kutoka mji wa Goma.