KINSHASA.Wafuasi wa Jean Pierre Bemba wapinga matokeo ya uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 15.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA.Wafuasi wa Jean Pierre Bemba wapinga matokeo ya uchaguzi

Wafuasi wa Jean Pierre Bemba mgombea wa kiti cha urais katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamepinga matokeo ya uchauzi yanayo onyesha kuwa rais Joseph Kabila anatarajiwa kushinda uchaguzi huo.

Chama cha mseto cha Union For the Nation kinacho muunga mkono Bemba kimeilaumu tume ya uchaguzi kwa kutumia udanganyifu katika kuhesabu kura.

Tume ya uchaguzi nchini Kongo imesema kuwa haitatangaza mshindi wa uchaguzi huo mpaka itakapo kamilisha uchunguzi wake kuhusu madai hayo.

Hali ya wasiwasi imetanda katika mji mkuu wa Kinshasa hasa baada ya vurugu za mwishoni mwa wiki zilizosababisha kuuwawa watu wanne.

Wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani na wale wa nchi za umoja wa ulaya wanadhibiti amani ili nchi hiyo isitumbukie tena katika machafuko.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com