Kinsahasa. Watu wawili wameuwawa katika mapigano ya vikosi vinavyounga mkono wagombea wa urais. | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinsahasa. Watu wawili wameuwawa katika mapigano ya vikosi vinavyounga mkono wagombea wa urais.

Raia wawili wameuwawa katika mapambano ya silaha baina ya wapiganaji wanaounga mkono wagombea wawili wa kiti cha urais katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

Mapigano hayo yalitokea karibu na makao ya makamu wa rais Jean-Pierre Bemba katika mji mkuu Kinshasa.

Bemba ni mgombea pamoja na rais wa sasa Joseph Kabila katika uchaguzi wa rais.

Matokeo kamili ya uchaguzi uliofanyika hapo Oktoba 29 wa duru ya pili bado hayajatolewa, lakini wanaomuunga mkono Bemba wamelalamika juu ya madai ya wizi wa kura.

Zaidi ya watu 20 wameuwawa katika mapigano baada ya uchaguzi wa kwanza hapo mwezi wa August.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com