KIEV:Mzozo wa kisiasa watokota nchini Ukraine | Habari za Ulimwengu | DW | 03.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV:Mzozo wa kisiasa watokota nchini Ukraine

Mvutano wa kisiasa nchini Ukraine unazidi kushika kasi, baada ya Rais Victor Yushchenko kutangaza kulivunja bunge, huku bunge nalo likigomea uamuzi huo.

Rais Yushchenko ametangaza tarehe 27 mwezi ujayo kuwa tarehe ya uchaguzi mpya.Lakini wabunge wa nchi hiyo wamepinga wakisema kuwa uamuzi huo ni kama mapinduzi ya kijeshi.

Bunge hilo la Ukraine pia limesema kuwa halitaridhia fedha za uchaguzi huo uliyoitishwa na Rais Yushchenko.

Rais Yushchenko anayeungwa mkono na nchi za magharibi, anamlaumu Waziri Mkuu anayeungwa mkono na Urusi, Viktor Yanukovych kujiongezea umaarufu zaidi kisiasa kitu ambacho anasema ni kwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Na habari za hivi punde zinasema kuwa maelfu ya wafuasi wa Waziri Mkuu huyo wameingia mitaani katika mji mkuu Kiev kupinga uamuzi wa Rais Yushchenko kulivunja bunge.

Wafuasi hao wameweka kambi nje ya jengo la bunge la Ukraine, ambapo wafuasi wa Rais Yushchenko nao wamesema kuwa wataweka kambi jirani na hapo.

Ukraine sasa inaingia katika mzozo mkubwa wa kisiasa toka vuguvugu la umma lililoiangusha serikali ya kikoministi mwaka 2004

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com