KIEV: Bunge la Ukraine lapunguza mamlaka ya Rais Viktor Yuschenko. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KIEV: Bunge la Ukraine lapunguza mamlaka ya Rais Viktor Yuschenko.

Rais Kikwete amaliza ziara yake nchini Burundi

Rais Kikwete amaliza ziara yake nchini Burundi

Wabunge wa Ukraine wamepiga kura kupunguza uwezo wa Rais Viktor Yuschenko, hatua inayochukuliwa kuwa pigo kubwa kwa utawala wake.

Wabunge mia tatu na sitini na sita kati ya wabunge mia nne na hamsini waliunga mkono sheria mpya inayompokonya rais mamlaka ya kukataa kumuidhinisha Waziri Mkuu anayechaguliwa na bunge.

Rais Viktor Yuschenko amepokonywa pia uwezo wa kumteua waziri wa ulinzi na pia waziri wa mambo ya nchi za nje.

Wengi wa wabunge wa kundi lililopitisha sheria hiyo ni wafuasi wa mpinzani wa Rais Viktor Yuschenko ambaye pia ni Waziri Mkuu Viktor Yanukovich na pia wafuasi wa mshirika wa zamani wa rais huyo, Yulia Timoshenko.

Rais Viktor Yuschenko alimshinda Viktor Yanukovich katika uchaguzi wa mwaka elfu mbili na nne lakini akalazimika kumteua kuwa waziri mkuu mwezi Agosti mwaka uliopita baada ya washirika wake kushindwa kuunda serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com