Kenya yaonya upinzani kuhusu kususia makampuni ya ′wafuasi′ wa Kibaki. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kenya yaonya upinzani kuhusu kususia makampuni ya 'wafuasi' wa Kibaki.

NAIROBI:

Serikali ya Kenya imeutaja uamuzi wa upande wa upinzani wa kuanzisha tena maandamano dhidi ya rais Mwai Kibaki pamoja na kususia makampuni ya wanaochukuliwa kuwa wafuasi wa Kibaki kama hujuma dhdid ya mashirika, kinyume cha sheria na tusi kwa waKenya.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ambayo imechapishwa leo. Taarifa imeendelea kuwaonya wanaisaisa kuwa watawjibika na yale yote yatakayotokea.

Kwa wakati huohuo machafuko ya mwishoni mwa juma yamesababisha watu watatu kufariki mjini Nairobi.Inasemekana kuwa watu walipigwa mapanga.

Na hayo yakiendelea Bw Raila Odinga ametarajiwa kuwasili mjini Kisumu leo kwa ibada ya kuwakumbuka wahanaga wa mashambulio amabyo yamesababisha watu 650 kufariki dunia na watu laki 2 unusu kuachwa bila makazi tangu Disemba mwaka jana.

Nae kamishna wa Umoja wa Ulaya- Louis Micheal – akiwa Nairobi amezitolea mwito pande zote zinazozana zifumbue mzozo wao kwa njia za mazungumzo.Odinga amesema atakutana na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan anaetazamiwa kuwasili kesho. Nae rais Yoweri Museveni wa Uganda ,mmoja wa vingozi wachache wa afrika aliempongeza raia Kibaki kwa kuchaguliwa tena, anatazamiwa kuwasili Nairobi kesho kwa juhudi za uptanishi ambazo upande wa upinzani wa Kenya unazitilia shaka kama hazitapendelea upande wowote.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com