Kashfa ya rushwa yasababisha waziri wa sheria wa Italia kujiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 17.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kashfa ya rushwa yasababisha waziri wa sheria wa Italia kujiuzulu

ROMA:

Waziri wa Sheria wa Italia –Clemente Mastella amejiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa.

Mastella ni mwana chama wa chama cha kikatiloki cha mrengo wa kati-cha Christian Democratic Party-UDEUR. Uchunguzi unaofanywa kuhusu rushwa, unawahusisha watu 23, akiwemo Mastella na mkewe mwana siasa Sandra Lonardo. Chama cha Mastella ni kidogo lakini muhimu kwa serikali ya waziri mkuu Romano Prodi.Viti witatu vya chama hicho, katika baraza la senate, vinampa wingi, japo mdogo, katika bunge la Italia.Na kwa mda huohuo mahakama ya kikatiba ya Italia imekubali kura ya maoni kuhusu mageuzi katika uchaguzi ambapo itavilazimu vyama vya siasa kupata wingi wa kura wa asili-mia 4 katika uchaguzi wa ngazi za taifa ili kupata uwakilishi katika bunge la kwanza ilhali asili mia nane katika baraza la Senate.

Chama cha Mastella kiliweza tu kushinda asili mia 1.4 ya uchaguzi mwaka wa 2006.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com