Kansela Merz alihutubia bunge mjini Berlin
29 Januari 2026
Matangazo
Kansela wa Ujerumani Fredrich Merz, amewataka viongozi wenzake barani Ulaya kushikamana na kujiweka kama kundi huru katika ulimwengu wenye utaratibu mpya unaozidi kuhodhiwa na Marekani, China na mataifa mengine yenye nguvu.
Katika hotuba yake mbele ya bunge mjini Berlin,kuhusu sera za nje za Ujerumani kiongozi huyo wa nchi, amesema Ulaya ni mbadala wa mitizamo ya kiimla na sera za kutumia mkono wa chuma duniani.
Merz asema Ujerumani haitojiunga sasa na Bodi ya Amani
Mtizamo wa Merz umetolewa wiki moja baada ya rais Donald Trump kulegeza msimamo kuhusu dhamira yake ya kukitwaa kisiwa cha Greenland.