Kansela Angela Merkel wa Ujerumani aukaribisha mwaka mpya 2009 kwa matumaini. | Masuala ya Jamii | DW | 01.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani aukaribisha mwaka mpya 2009 kwa matumaini.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani aukaribisha mwaka mpya wa 2009 kwa matumaini na kwa ahadi ya kuchochea uchumi na kushinikiza mashirika ya kimataifa na kuanzisha taratibu kali za kusimamia masuala ya fedha duniani.

default

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani muda mfupi kabla ya kuwasilisha hotuba yake ya mwaka mpya wa 2009.

Wapenzi wananchi mabibi na mabwana.

Kumalizika kwa mwaka ni wakati muhimu na pia sio muhimu kutengana nao.Kitu gani kilikuwa muhimu kwako kwa mwaka huo?Matakwa yako ya muda mrefu yameweza kutimizwa?Tatizo la wapenzi wananchi ? Kuzaliwa kwa watoto wenu?Mustakbali wa maisha yenu ya kazi?Wakati wa kuwa na familia na marafiki?

Merkel katika hotuba yake hii anasema atashinikiza kuwepo taratibu kali za kimataifa za kusimamia masuala ya fedha kwa kusema kwamba mgogoro wa kiuchumi duniani umetowa fursa ya kuwepo kwa udhibiti zaidi na uwazi mkubwa zaidi.

Anasema serikali yake itaongeza matumizi katika miundo mbinu na elimu ili kuchohea ukuaji wa uchumi lakini anaonya kwamba hatoshinikizwa katika kuruhusu matumizi makubwa sana ili kuchochea uchumi.

Dunia imejifunza kutokana na mgogoro huo wa fedha na kwamba matumizi ya kupindukia ya kifedha na tabia ya kutowajibika ya baadhi ya wanamabenki na mameneja ni mambo yanayopaswa kulaumiwa kwa mgogoro huo.Anasema dunia imeishi kupindukia uwezo wake kwa hiyo atayashinikiza mashirika ya kimataifa katika kuweka udhibiti mkali wa masuala ya fedha.

Anasema fursa ilioletwa na mgogoro huo wa fedha duniani ni kuanzishwa kwa sheria za kimataifa ambazo zitazingatia misingi ya uchumi unaotegmea nguvu za soko la jamii na kwamba hatoregeza kamba hadi hapo watakapofanikisha lengo lao la kuweka sheria hizo.

Merkel anasema taifa ni mlezi wa utaratibu wa uchumi wa jamii na ushindani lazima uwe na hisia ya uwiano wa uwajibikaji wa kijamii ambayo ni misingi ya uchumi wa nguvu za soko la kijamii inayotumika nchini Ujerumani lakini anasema haitoshi na kwamba lazima misingi hiyo ya muongozo ifuatwe duniani kote.

Merkel pia anasema serikali itatanuwa barabara na njia za reli na kuboresha mawasiliano pamoja na kuhifadhi na kuongeza ajira.Shule,vituo vya mafunzo na vyuo vikuu vitapewa kipau mbele katika matumizi mapya ya serikali.

Anaongeza kusema kwamba Ujerumani ambayo haikuathirika sana na mgogoro huo wa fedha kama nchi nyengine haitoshinikizwa katika kuchukuwa hatua za kuchochea uchumi za kiwango sawa na zile za nchi nyengine.

Anasema serikali inachukuwa hatua kwa nia na kwa ushindani lakini hatochukuwa uamuzi wowote ule kwa kuzingatia nani anayepiga kelele kwa nguvu zaidi.

Mwisho Kansela Merkel amewatakia wanachi wake wote heri na baraka za mwaka mpya wa 2009.

 • Tarehe 01.01.2009
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GQ7y
 • Tarehe 01.01.2009
 • Mwandishi Mohamed Dahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GQ7y
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com