Kansela ahimiza kanuni mpya za masoko | Habari za Ulimwengu | DW | 29.03.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Kansela ahimiza kanuni mpya za masoko

Kansela Merkel atetea msimamo wa serikali yake kuzinusuru benki zisifilisike


Berlin:

Kansela Angela Merkel ametoa mwito kwa mara nyengine tena wa kutiwa njiani kanuni imara katika masoko ya fedha.Kansela Merkel amewaambia wajumbe waliohudhuria mkutano wa chama chake cha Christian Democratic Union -CDU mjini Berlin,masoko ndiyo ya kulaumiwa katika mgogoro wa sasa wa kiuchumi .Kansela Angela Merkel ametetea pia uamuzi wa serikali yake wa kudhamani benki zenye shida mfano wa Hypo Real Estate.Kansela Angela Merkel amesema ikiwa utaratibu wa masoko kujiendesheya mambo yao wenyewe umeshindwa,lazma serikali iingilie kati.Kansela Angela Merkel amesema hayo siku chache kabla ya mkutano wa kilele wa mataifa tajiri kiviwanda na yale yanayoinukia G-20 mjini London nchini Uengereza-ambapo viongozi wanapanga kusaka njia ya kupatia ufumbuzi mgoghoro wa kiuchumi na fedha unaoikaba dunia.

 • Tarehe 29.03.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HMHw
 • Tarehe 29.03.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HMHw
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com