KAMPALA:Waasi wa LRA wawasili Kampala bila ya hofu | Habari za Ulimwengu | DW | 01.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KAMPALA:Waasi wa LRA wawasili Kampala bila ya hofu

Wawakilishi wa kundi la waasi wa LRA wamewasili karibu na mji wa Kampala kwa mara ya kwanza bila ya kuwa na hofu juu ya kukamatwa.

Wawakilishi hao wanaandamana na wapatanishi kutoka kwenye mazungumzo yanayofanyika kusini mwa Sudan.

Mazungumzo hayo ni juu ya kusuluhisha mgogoro wa kaskazini mwa Uganda baina ya majeshi ya serikali na waasi hao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com