Kampala.Ripoti ya Umoja wa Mataifa yailaumu serikali ya Uganda kwa mauaji ya wanavijiji. | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kampala.Ripoti ya Umoja wa Mataifa yailaumu serikali ya Uganda kwa mauaji ya wanavijiji.

Umoja wa Mataifa umesema hii leo, Jeshi la Uganda lilifurutu ada katika operesheni yake ya hivi karibuni dhidi ya vijiji vilivyojengwa kinyume na sheria kaskazini mwa Uganda, ambapo watu wasio pungua 55 wakiwemo wanawake na watoto wameuwawa.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia haki za binaadamu Louise Arbour ameitaka serikali isitishe kampeni yake ya miezi sita ya kuwapokonya silaha wanamgambo na makundi ya wahalifu, hadi itakapohakikisha kwamba operesheni hiyo haitakuwa na madhara kwa raia.

Ripoti hiyo ya tume ya utafiti imesema wengi kati ya watu waliouliwa mwishoni mwa mwezi wa October, wamekufa kutokana na kufyetuliana risasi kati ya wanajeshi na wana vijiji, lakini watu sita waliuliwa kikatili na wanajeshi.

Aidha ripoti hiyo pia inalituhumu jeshi , kwa kuwakamata watu 68 kinyume na sheria, kuwatesa watu 14, kumbaka bibi mmoja mtu mzima na kuzitia moto zaidi ya nyumba 200.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com