KABUL: Vikosi vya Marekani vyalaumiwa kuua raia 8 Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Vikosi vya Marekani vyalaumiwa kuua raia 8 Afghanistan

Maelfu ya watu wameandamana mjini Jalalabad, mashariki mwa Afghanistan wakilalamika dhidi ya mauaji ya hadi raia 8.Waandamanaji wanasema,raia hao waliuawa na vikosi vya Kimarekani vilivyofyatua risasi bila ya kuchagua.Vile vile raia wengine wasiopungua 35 walijeruhiwa kwa risasi za Marekani,kufuatia kile kilichoelezwa na maafisa wa kijeshi kuwa ni shambulio la utata lililofanywa na wanamgambo.Maafisa hao wamesema, vikosi vya Kimarekani vilifyatua risasi baada ya mlolongo wa magari yao kushambuliwa na mshambulizi aliejitolea muhanga katika gari iliyopakiwa miripuko na baadae vikafyatuliwa risasi kutoka pande mbali mbali.Vikosi vya Marekani na vya washirika wake,vimeahidi kulichunguza tukio hilo,lakini vimesisitiza kuwa baadhi kubwa ya vifo hivyo huenda ikawa vimesababishwa na wanamgambo.Kwa upande mwingine, wanajeshi 2 wa Kingereza wameuawa katika mapigano yaliozuka katika wilaya ya Helmand,kusini mwa Afghanistan.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com