KABUL: Mamia ya wanamgambo wa Taliban washambulia na kudhibiti mji wa kusini mwa Afghanistan. | Habari za Ulimwengu | DW | 03.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Mamia ya wanamgambo wa Taliban washambulia na kudhibiti mji wa kusini mwa Afghanistan.

Mamia ya wanamgambo wa Taliban wameshambulia na kuudhibiti mji wa Musa Qala, mji ambao wanajeshi wa Uingereza waliuondoka mwaka uliopita na kuwaachia viongozi wa kikabila kusini mwa Afghanistan.

Duru zinasema wanamgambo hao walinyakua silaha kutoka kwa polisi na pia wakaharibu makao makuu ya serikali katika mji huo.

Wakazi wanasemekana wamekuwa wakikimbia kutoka eneo hilo wakiogopa huenda majeshi ya NATO yakawashambulia kwa mabomu wanamgambo hao wa Taliban.

Maafisa wa NATO wamesema inaonekana kama kwamba wanamgambo hao walivamia makao hayo makuu ya serikali kulipiza kisasi cha shambulio la angani la juma lililopita lililosababisha kuuawa jamaa mmoja wa kiongozi wa kundi hilo la Taliban.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com