KABUL: Majeshi ya NATO na Afghanistan yawaua wanamgambo wa 150 wa Taliban. | Habari za Ulimwengu | DW | 11.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Majeshi ya NATO na Afghanistan yawaua wanamgambo wa 150 wa Taliban.

Majeshi ya NATO pamoja na Afghanistan yamewauwa wanamgambo takriban mia moja na hamsini walioonekana wakati wa usiku wakiingia nchini humo wakitokea Pakistan.

Majeshi ya NATO yametoa taarifa iliyosema wanamgambo hao walionekana mpakani wakiwa na mipango ya kuvishambulia vikosi vya Afghanistan.

Wanamgambo hao waliojigawa katika makundi mawili waliandamwa na kushambuliwa kutoka hewani na pia na majeshi ya nchi kavu katika mpaka, kwenye jimbo la mashariki la Pakistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com