Juhudi za uokoaji zinaendelea nchini Italia. | Masuala ya Jamii | DW | 07.04.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Juhudi za uokoaji zinaendelea nchini Italia.

Juhudi za uokoaji zinaendelea kujaribu kuwatafuta watu walionusurika, baada ya tetemeko la ardhi katika mji wa L'Aquila Italia jana na lilosababisha vifo vya watu 179, huku wengine wakiachwa bila ya makazi.

Madhara ya Tetemeko la ardhi, lililotokea jana katika mji wa L'Aquila, nchini Italia

Madhara ya Tetemeko la ardhi, lililotokea jana katika mji wa L'Aquila, nchini Italia

Waokoaji wamekuwa wakitumia mashine za kuchimbua na kwa mikono yao kutafuta watu hao waliokumbwa na tetemeko hilo baya kabisa kutokea nchini Italia kwa kipindi cha miongo mitatu iliyopita.


Waokoaji hao wanasema kuwa zaidi ya saa 24, tangu kutokea kwa tetemeko hilo, watu 34 bado hawajulikani walipo.


Siku moja baada ya tetemeko hilo kukumba jimbo la Abruzzo, Waokoaji walifanikiwa kuwatoa katika kifusi wanafunzi wawili mapema leo kutoka katika jengo lililoporomoka katika mji wa kihistoria wa L'Aquila unaokaliwa na wakazi wapatao elfu 68.


Waokoaji tayari wamewaokoa watu 100 wakiwa hai, kutoka katika vifusi, lakini hata hivyo watu wengine 250, wanaaminika kuwa hawaonekani, huku matumaini ya kupatakana wengi wao wakiwa hai yakiwekwa.


Waziri Mkuu wa nchi hiyo Silvio Berlusconi ambaye ametangaza hali ya hatari na kutembelea eneo la tukio, amesema watu 150 wamekufa na wengine zaidi ya elfu moja na 500 wamejeruhiwa.


Amesema janga hilo ni kubwa na watapaswa kujenga upya hali ambayo itahitaji kiasi kikubwa cha fedha na kuahidi kutafuta mamilioni ya Yuro katika mfuko wa majanga wa Umoja wa Ulaya.


Watu wengine elfu 50 wanadaiwa kupoteza makazi yao kutokana na shambulio hilo.


Wakati janga hilo kubwa likiikumba nchi hiyo na juhudi za uokoaji zikiendelea, Polisi nchini humo wamearifiwa kufanya doria katika nyumba ambazo ziliharibiwa na kubaki wazi kutokana na tetemeko hilo na kuwakamata watu kadhaa waliokuwa waiiba vitu.


Maelfu ya mahema katika maeneo ya bustani na viwanja vya mpira kuweza kuwahifadhi watu hao waliopoteza makazi yao.


Watu kadhaa wameripotiwa kulala katika magari, baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuwataka watu wasirudi manyumbani mwao, kwani ni hatari.


Baadhi ya watu walionusurika katika tetemeko hilo wamelielezea kama shambulio la bomu akati wa usiku na uchungu wa kutojua majaliwa ya wapendwa wao.


Tetemeko hilo ni baya kulikumba Italia tangu Novemba mwaka 1980 baada ya tetemeko lenye kipimo cha 6.5 kuua wat elfu 2735.


Tayari salamu za rambirambi zimeanza kutolewa kutoka sehemu mbalimbali duniani huku huku wapinzani wa kisiasa nchini humo wakiweka tofauti zao chini na kuomboleza kwa pamoja.

 • Tarehe 07.04.2009
 • Mwandishi Halima Nyanza/AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HRm5
 • Tarehe 07.04.2009
 • Mwandishi Halima Nyanza/AFP
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/HRm5
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com