Joto la uchaguzi mkuu linazidi nchini Kenya | Matukio ya Kisiasa | DW | 20.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Joto la uchaguzi mkuu linazidi nchini Kenya

Nchini Kenya joto la kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu linazidi huku kila mwamba ngoma akivutia upande wake.

Mwenyekiti wa chama cha Kaddu na mshirika wa karibu wa rais wa zamani Daniel Arap Moi na pia aliyewahi kuwa waziri katika utawala wa Moi Cyrus Jirongo ametangaza kumuunga mkono mgombea wa chama cha ODM Raila Odinga hatua ambayo inatofautiana na ile ya rais Kibaki.

Katika chama cha ODM kenya Kalonzo Musyoka amemteua Julia Ojiambo kuwa mgombea wake mwenza huku kukiwa na habari kwamba juhudi zinaendelea kuzitaka ODM mbili kufikia muafaka wa ushirikiano kuimarisha nguvu za upinzani kukabiliana na raia Kibaki.

Saumu Mwasimba alizungumza na Julia Ojiambo na kwanza akieleza juu ya hisia zake baada ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa Kalonzo Musyoka.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com