JOHANNESBURG: Mkuu wa polisi wa zamani ahukumiwa kifungo cha nje | Habari za Ulimwengu | DW | 18.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG: Mkuu wa polisi wa zamani ahukumiwa kifungo cha nje

Aliekuwa waziri wa sheria na utulivu wa Afrika Kusini,Adriaan Vlok na polisi wanne,wamehukumiwa kifungo cha nje kwa makosa ya kupanga njama ya kutaka kumuuwa mwanaharakati aliepinga utawala wa ubaguzi wa rangi.Washtakiwa hao watano walikiri makosa ya kutaka kumuua Mchungaji Frank Chikane, kwa kutia sumu katika chupi yake.

Kesi hiyo inatazamwa kama mtihani wa kesi za maafisa wa enzi ya ubaguzi wa rangi,ambao hawakusamehewa na Tume ya Ukweli na Upatanisho nchini humo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com