Jeshi la Marekani lasema laua wanamgambo 38 mjini Baghdad | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Jeshi la Marekani lasema laua wanamgambo 38 mjini Baghdad

Eneo la Green Zone limeshambuliwa kwa mizinga siku ya pili mfululizo

default

Wapiganaji wa jeshi la Mahdi wakiwa katika kiunga cha mji wa Baghdad cha Sadr City, Iraq, Jumamosi, March 29, 2008. Takriban wapiganaji hao 38 wameuawa na jeshi la Marekani mwishoni mwa juma walipovishambulia vikosi vyake mjini humo wakitumia dhoruba la mchanga lililotanda Baghdad kama kificho.

Jeshi la Marekani linasema kuwa vikosi vya Iraq vikisaidiwa na vya Marekani vimewauwa wapiganaji 38 katika mapigano makali mjini Baghdad.Miongoni mwa hao waliouawa,jeshi linasema, 22 walikuwa wale walioshambulia kituo cha kijeshi katika mtaa wa waShia.

Jeshi la Marekani limesema leojumatatu kuwa limeanzisha tena hujuma kali dhidi ya wapiganaji ambao walishambulia vikosi vya Marekani na Iraq katika eneo la Mashariki mwa jiji la Baghdad mwishoni mwa juma.Katika mapigano yaliyofuata,kwa mujibu wa jeshi la Marekani, ni vifo vya ambao limewaita majangili 38. Hujuma za sasa zimekuja huku juhudi mpya za kisiasa zikianzishwa ili kumaliza umwagikaji wa damu.

Mapigano ya jana jumapili yalikuwa makali sana, kulingana na jeshi la Marekani.Wapiganaji hao inasemekana sio tu waliwashambulia wanajeshi kwa kutumia bunduki za mkono lakini pia walilivurumishia eneo linalolindwa sana mjini Baghdad la Green Zone mizinga ,wakitumia nafasi ya dhoruba la mchanga ambalo lilikuwa limetanda na hivyo kuzuia kuruka kwa ndege za kijeshi za Marekani kuweza kuwashambulia.

Habari zaidi zasema kuwa leo asubuhi wapiganaji hao pia wamevurumisha tena makombora mengine katika eneo la Green zone la mjini Baghdad.Ubalozi wa Marekani umehakikisha kuwa eneo hilo limeshambuliwa na kuongeza kuwa hakuna aliejerihiwa ama kuaawa.

Eneo hilo linalopatikana upande wa magharibi wa mto Tigris ndiko kunapatikana ofisi za serikali ya Iraq pamoja na balozi za Marekani na Uingereza.

Kutokana na hali kuwa mji wa Baghdad umefunikwa na dhoruba ya mchanga na hivyo kuwa vigumu kwa ndege za kijeshi za Marekani kufanya doria kamili na pia kufanya mashambulizi,jeshi la marekani linasema limeanzisha hujuma kali dhidi ya washambulizi kwa kutumia vifaru pamoja na magari mengine ya deraya.

Mapigano mengi yalitokea katika eneo la Sadr City la mji wa Baghdad ambako ndiko kunapatikana kwa wingi wanamgambo watiifu kwa kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali Muqtada al -Sadr.Wapiganaji hao wanajiita jeshi la Mahdi.

Kiongozi huyo wa kidini anasema kuwa wapiganaji wake wanalengwa kimakusudi.

Lakini makamanda wa jeshi la Marekani na la Iraq kwa upande wao,wanasema wanajaribu kukomesha uvurumishwaji wa makombora kwa eneo la Green Zone ukitokea katika Sadr City.Marekani inailaumu Iran kwa kuwasaidia wapiganaji hao na kuongeza kuwa wapiganaji hao wanatumia silaha kutoka Iran.Iran kwa upande wake inakanusha kuhusika.

Katika mapigano haya mapya watu wasiopungua 38 wameuawa.

Vifo hivyo sasa vinajumulisha vifo vya watu,wakiwemo wanamgambo pamoja na raia wa kawaida 440 ambao wameuawa katika mapigano yaliyodumu mwezi sasa katika mtaa wa Sadr City,ambako ghasia zilizuka kufuatia agizo la Waziri Mkuu Nuri-al-Maliki la kuwashughulikia wanamgambo.Agizo hilo la Machi 25 lilianzia katika mji wa kusini wa Basra.

Tangu ghasia hizo zianze takriban wanajeshi wa Marekani 15 wameuawa.

Huku hayo yakiendelea ofisi ya kiongozi wa kidini Muqtada Sadr ilioko katika mji mtakatifu wa Najaf inasema kuwa juhudi mpya zimeanzishwa na rais Jalal Talaban kujaribu kumaliza mgogoro kati ya kundi la Sadr na serikali.

Kundi la Sadr limekataa masharti ya waziri mkuu al Maliki ya kumaliza mapigano jumapili.

Al- Maliki,katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni mwishioni mwa juma, ametoa masharti manne ya kumaliza kamatakamata ya kundi la jeshi la Mahdi. Miongoni mwa hayo ni kuwa silaha zote kubwa zikabidhiwe kwa serikali,kuwa kundi hilo lisiingilie tena shughuli za serikali au za idara za serikali kama vile polisi na jeshi na pia washukiwa wakabidhiwe kwa vyombo vya usalama.

 • Tarehe 28.04.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dpsl
 • Tarehe 28.04.2008
 • Mwandishi Kalyango Siraj
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dpsl
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com