1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM : Rais Katsav wa Israel ajiuzulu

29 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnN

Rais wa Israel Moshe Katsav amejiuzulu leo hii baada ya kukubali mpango wa makubaliano tata wa kukiri ambao unamwezesha kuepuka kujibu madai ya ubakaji.

Rais huyo aliwasilisha hati ya kujiuzulu kwake kwa bunge la Israel Kneset.

Mpango wa makubaliano hayo ambayo kwayo Katsav amekiri makosa mengine ya unyanyasaji wa kingono na vitendo vya aibu umetangazwa hapo jana na Mwanasheria Mkuu wa serikali Meni Mazuz.Hapo mwezi wa Januari Mazuz amesema alikuwa amepanga kumshtaki Katsav kwa madai ya ubakaji na uhalifu mwengine wa ngono makosa ambayo yangeliweza kupelekea kufungwa gerezani kwa miaka 20.

Makubaliano hayo ambayo Katsav amekubali kifungo cha nje na faini ya dola 11,000 yamelaaniwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa haki na watu wanaodai kutendewa madhila hayo na Katsav pamoja na makundi ya kutetea haki za binadamu.