Jeribio kutenzua mgogoro wa Colombia na majirani wawili | Habari za Ulimwengu | DW | 06.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Jeribio kutenzua mgogoro wa Colombia na majirani wawili

WASHINGTON:

Jumuiya ya Nchi za Bara la Amerika OAS imepitisha azimio linalojaribu kupunguza mvutano kati ya Colombia na majirani wake wawili-Ecuador na Venezuela.Azimio hilo linasema,Colombia ilikiuka uhuru wa mipaka ya Ecuador,ilipofanya mashambulizi katika ardhi ya nchi hiyo mwisho wa juma lililopita na kumuua kiongozi mwandalizi wa kundi la waasi la FARC.Lakini azimio hilo halikuilaani Colombia kwa operesheni hiyo ya kijeshi.

Wanachama wa OAS mjini Washington,wamekubali kuzindua halmashauri itakayochunguza tukio hilo.Ecuador na Venezuela imejibu shambulizi la Colombia kwa kusitisha kwa muda uhusiano wa kibalozi pamoja na serikali ya Bogota.Mataifa hayo mawili vile vile yameimarisha vikosi kwenye mipaka yake na Colombia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com