Japan kutetea taji la Dunia dhidi ya Marekani | Michezo | DW | 04.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Japan kutetea taji la Dunia dhidi ya Marekani

Miaka minne iliyopita wakati wachezaji wa Japan walinyanyua Kombe la Dunia la Wanawake, taifa lilisherehekea. Kabla ya ushindi huo Ujerumani, Japan ilikuwa imesambaratishwa na tetemeko kubwa la ardhi na Tsunami

Timu ya taifa iliipa nchi hiyo sababu ya kushangilia, na wachezaji wakakaribishwa nyumbani kama mashujaa. Wanawake hao walishinda taji la kwanza kabisa la Kombe la Dunia kwa kuwaangusha miamba Marekani kwa mikwaju ya penalty baada ya kutoka sare ya mbili mbili.

Sasa Wajapan watakutana tena na Marekani katika fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake. Mara hii nchini Canada. Ikiwa watapata ushindi, japan watakuwa timu ya pili kuwahi kurudia kama mabingwa wa Kombe la Dunia baada ya Ujerumani (2003 na 2007) katika vinyang'anyiro viwili mfululizo vya Kombe la Dunia. Marekani inatafuta taji lake la tatu, lakini la kwanza tangu mwaka wa 1999. Abby Wambach ni mchambuaji wa Marekani

Kabla ya fainali, England na Ujerumani zitafuta machozi katika mchuano kumtafuta mshindi wa tatu leo usiku. Siyo mchuano wa mwisho ambao kila timu ilitarajia kuucheza lakini baada ya mwezi mmoja wa kandanda safi wenye hisia za kila aina kufikia katika nusu fainali, timu zote mbili zinalenga kumaliza dimba la Kombe la Dunia la Wanawake kwa tabasamu.

Kwa kocha wa Ujerumani Silvia Neid, huu utakuwa mchuano wake wa 17 katika dimba la Kombe la Dunia. Pia ni Kombe la Dunia la mwisho kwa Neid ambaye atajiuzulu baada ya Michezo ya Olimpiki mwaka ujao.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu