Israel yachunguza visa vya jeshi lake dhidi ya wanamaji wa Ujerumani katika fukwe za Libnan | Habari za Ulimwengu | DW | 12.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Israel yachunguza visa vya jeshi lake dhidi ya wanamaji wa Ujerumani katika fukwe za Libnan

Tel Aviv:

Jeshi la Israel limesema linachunguza ripoti za visa vinavyosemekana vimetokea dhidi ya wanajeshi wa Ujerumani wanaotuimikia vikosi vya Umoja wa mataifa katika fukwe za Libnan.Madege kadhaa ya kijeshi ya Israel yanasemekana yaliiandama manuari ya kijeshi ya Ujerumani “NIEDERSACHEN” jumatano iliyopita. Tukio kama hilo liliripotiwa pia April 30 iliyopita ambapo mashua za kijeshi za Israel zilipita kwa kasi na kuikaribia manuari ya kijeshi bila ya kutoa ishara yoyote.Makao makuu ya vikosi vya Umoja wa mataifa yameshaarifiwa kuhusu visa vyote hivyo viwili.Wanamaji wa Ujerumani wanatumikia vikosi vya kulinda amani za umoja wa mataifa –UNIFIL tangu october iliyopita-katika fukwe za Libnan

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com