1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Ujumbe watumwa kujadiliana na viongozi wa kidini.

9 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkQ

Serikali ya Pakistan imetuma ujumbe katika msikiti uliozingirwa ili kujaribu kupata makubaliano juu ya kumalizika kwa mkwamo wa siku saba sasa na wapiganaji wenye silaha.

Ujumbe huo unaongozwa na waziri mkuu wa zamani Chaudhry Shujaat Hussain na pia unajumuisha viongozi wakuu wa kidini. Waziri wa habari Mohammed Ali Durrani amesema kuwa bado kuna nafasi nyingi za kutatua mzozo huo.

Abdul Rashid Ghazi, kiongozi wa kidini ambaye anaongoza upinzani huo wa msikiti , anaripotiwa kuwa amekubali kuwa na mazungumzo na ujumbe huo.

Serikali inawashutumu wanaharakati hao kwa kuwazuwia wanawake na watoto na kuwatumia kama ngao katika msikiti.

Hadi sasa , zaidi ya watu 20 wameuwawa tangu jeshi lizingire msikiti huo na mapigano yalizuka wiki iliyopita.