GHAZNI:Muda wa mwisho uliowekwa na Taleban upo karibu kwisha | Habari za Ulimwengu | DW | 31.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GHAZNI:Muda wa mwisho uliowekwa na Taleban upo karibu kwisha

Kundi la Taleban nchini Afghanistan wanaipa serikali nchini humo muda mpya wa mwisho hadi kesho asubuhi saa oja asubuhi saa za London ili madai yao kutimizwa kwa madhumuni ya kuwaokoa mateka 21 wa Korea Kusini waliosalia .Hatua hii inatokea siku moja baada ya mateka wa pili kuuawa.Kundi la Taleban linaitaka serikali kuwaachia huru yapata wafungwa wao 8 wanaozuiliwa kwenye magereza nchini Afghanistan jambo ambalo Rais Hamid Karzai wa Afghanistan anapinga.

''Nadhani kimsingi hatupaswi kuunga mkono utekaji nyara kwa kutimiza madai yao.''

Mwili wa mateka aliouliwa hapo jana umepatikana kwenye eneo lililo kusini mwa mkoa wa Ghazni ukiwa na majeraha ya risasi.Wizara ya mambo ya nje imetambua jina la maiti hiyo ambalo ni Shim Sung-Min aliyekuwa na umri wa miaka 29.

Mwili wa kasisi aliyeongoza kundi hilo Bae Hyung-Kyu ulipatikana katika eneo hilohilo jumatano iliyopita.Kundi hilo lilikuwa katika shughuli za kutoa misaada katika eneo la kusini mwa Afghanistan lililo na usalama duni. Kwa mujibu wa serikali juhudi za kuendelea kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia zinaendelea.

Mateka hao wa Korea Kusini ni wa kanisa la kiinjilisti na walikamatwa walipokuwa msafarani kuelekea mjini Kabul yapata wiki mbili zilizopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com